• HABARI MPYA

    Sunday, April 29, 2018

    REFA NIGERIA AFUNGIWA MWAKA KWA KUTAKA KUPANGA MATOKEO

    KAMATI ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imethibitisha adhabu ya Kamati yake ya Nidhamu kumfungia mwaka mmoja, refa Joseph Ogabor wa Nigeria kutojihusisha na soka kwa tuhuma za kushawishi upangwaji wa matokeo ya mechi.
    Taarifa ya CAF iliyotoka jana imesema kwamba refa huyo aliwashawishi waamuzi wa mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Plateau United ya Nigeria na USM Alger ya Algeria uliochezwa Aprili 7 mwaka huu mjini Lagos wapange matokeo.
    Uamuzi huo umefuatia uchunguzi uliofanywa pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa na marefa wa Afrika Kusini ambao walisema waliombwa na Ogabor kuisaidia timu ya Nigeria ishinde.
    Aidha, Plateau United imeonywa kwa tabia ya kuwapa zawadi na kuwafanyia ukaribu marefa ili wawavutie kuwasaidia kushinda mechi.
    Pamoja na hayo, Chama cha Soka Afrika Kusini (SAFA) kimetakiwa kuwaomba radhi Shirikisho la Soka Nigeria (NFF) baada ya uchunguzi kuthibitisha hakukuwa na hongo ya dola za Kimarekani 30,000 iliyotolewa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REFA NIGERIA AFUNGIWA MWAKA KWA KUTAKA KUPANGA MATOKEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top