• HABARI MPYA

    Friday, April 20, 2018

    KAZI IPO LEO KAMBARAGE STAND UNITED NA MTIBWA SUGAR NUSU FAINALI ASFC

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    NUSU Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) inatarajiwa kufanyika leo Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga ikizikutanisha wenyeji, Stand United na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
    Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila ni mwenye matumaini makubwa kuelekea kwenye mchezo hyo, akiamimi timu yake itawafunga wenyeji na kwenda Fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia yao.
    Katwila amesema kwamba wachezaji wote muhimu wa Mtibwa Sugar wako fiti na tayari kwa mchezo wa leo, akiwemo kiungo Hassan Dilunga ambaye alikuwa majeruhi.
    “Wachezaji wote wapo fiti, hata Dilunga ambaye alikuwa ana maumivu kidogo baada ya kuumia mazoezini, naye anaendelea vizuri na kwa ujumla lengo letu ni ushindi ili kusonga mbele,”amesema Katwila.
    Kwa upande wake, Kocha Msaidizi wa Stand United, Athumani Bilal amesema kwamba kwamba namna yoyote Mtibwa Sugar watapigwa leo Kambarage.
    “Mtibwa Sugar ni timu nzuri, lakini leo tunawapiga kwa sababu watakutana na timu nzuri zaidi yao na isitoshe pia sisi tumejipanga lengo letu ni kucheza mechuano ya Afrika mwakani,”alisema Bilal ‘Bilo’.   
    Nusu Fainali ya pili Azam Sports Federation Cup itafuatia Jumatatu Uwanja wa Namfua mjini Singida, ikizikutanisha JKT Tanzania ya Dar es Salaam na wenyeji Singida United.
    Fainali ya michuano hiyo itafanyika Juni 2, mwaka huu Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha na bingwa pamoja na kupata Sh. Milioni 50, pia ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
    Mshindi wa pili atapata Milioni 10, wakati Mchezaji Bora atazawadiwa Sh. Milioni 1 sawa na Kipa Bora, Mfungaji Bora, huku Mchezaji Bora wa Fainali akiondoka na Sh. 500,000. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAZI IPO LEO KAMBARAGE STAND UNITED NA MTIBWA SUGAR NUSU FAINALI ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top