• HABARI MPYA

    Saturday, April 21, 2018

    YANGA SC YAPANGWA NA WAALGERIA, RAYON SPORT NA GOR MAHIA KOMBE LA SHIRIKISHO

    Kundi A; ASEC Mimosas (Ivory Coast), Raja Club Athletic Morocco), AS Vita (DRC) na Aduana (Ghana).
    Kundi B; RS Berkane (Morocco), El Masry (Misri), UD Songo (Msumbiji) na El Hilal (Sudan).
    Kundi C; Enyimba (Nigeria), Williamsville (Ivory Coast), CARA (Kongo) na Djoliba (Mali)
    Kundi D; Rayon Sports (Rwanda), USM Alger (Algeria), Yanga SC (Tanzania) na Gor Mahia (Kenya).

    Na Mwandishi Wetu, CAIRO
    YANGA SC imepangwa Kundi D pamoja na USM Alger ya Algeria, Rayon Sport ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya katika hatua ya 16 Bora ya Kombe Shirikisho Afrika.
    Katika Droo ya hatua ya makundi iliyopangwa leo mjini Cairo, Misri Kundi A lina timu za ASEC Mimosa ya Ivory Coast, Raja Club Athletic, maarufu Raja Casablanca ya Morocco, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Aduana Stars ya Ghana.
    Kundi B linaundwa na RS Berkane ya Morocco, Al Masry ya Misri, UD Songo ya Msumbiji na El Hilal ya Sudan, wakati Kundi C lina timu za CARA ya Kongo, Enyimba ya Nigeria, Williamsville na Djoliba ya Mali.
    Droo hiyo iliongozwa na Katibu Mkuu wa CAF, Amr Fahmy na Katibu Msaidizi, Anthony Baffoe.
    Yanga itaanzia ugenini hatua ya makundi kwa kumenyana na USMA Alger nchini Algeria Mei 6, kabla ya kumenyana na Rayon Sport mjini Dar es Salaam Mei 16 na itakamilisha mechi za mzunguko wa kwanza kwa kuwafuata Gor Mahia mjini Nairobi Julai 18.
    Mzunguko wa pili Yanga itaanzia nyumbani Julai 29 na Gor Mahia, kabla ya kuwakaribisha na USMA Alger Agosti 19 na kwenda kumalizia ugenini Agosti 29 na Rayon.

    RATIBA YA MECHI ZA YANGA KUNDI D
    Mei 6, 2018: USMA v Yanga, Algiers
    Mei 16, 2018: Yanga v Rayon, Dar Es Salaam
    Julai 18, 2018: Gor Mahia v Yanga, Nairobi 
    ----------------------------------------
    Julai 29, 2018: Yanga v Gor Mahia, Dar es Salaam
    Agosti 19, 2018: Yanga v USMA, Dar es Salaam

    Agosti 29, 2018: Rayon v Yanga, Kigali
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAPANGWA NA WAALGERIA, RAYON SPORT NA GOR MAHIA KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top