• HABARI MPYA

    Monday, April 23, 2018

    SINGIDA UNITED YAIFUATA MTIBWA SUGAR FAINALI KOMBE LA TFF…YAIPIGA 2-1 JKT

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Singida United imefanikiwa kuingia Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania Uwanja wa Namfua mjini Singida.
    Haukuwa ushindi mwepesi kwa Singida, kwani ililazimika kutoka nyuma kwa bao 1-0 na kumaliza kwa sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 kabla ya kwenda kushinda 2-1 katika dakika 30 za nyongeza.
    JKT Tanzania ilitangulia kwa bao la mshambuliaji wake hatari, Hassan Matalema dakika ya 38, kabla ya Tafadzwa Kutinyu kuisawazishia Singida United dakika ya 54.
    Mchezo ukahamia kwenye dakika 30 za nyongeza baada ya dakika 90 kumalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1 na mshambuliaji kutoka Zimbabwe, Kutinyu akaifungia bao la ushindin Singida United dakika ya 98.
    Singida United itacheza fainali Juni 2, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha dhidi ya Mtibwa Sugar iliyoitoa Stand United kwa kuwachapa 2-0 mjini Shinyanga Ijumaa. 
    Bingwa pamoja na kupata Sh. Milioni 50, pia ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
    Mshindi wa pili atapata Milioni 10, wakati Mchezaji Bora atazawadiwa Sh. Milioni 1 sawa na Kipa Bora, Mfungaji Bora, huku Mchezaji Bora wa Fainali akiondoka na Sh. 500,000. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA UNITED YAIFUATA MTIBWA SUGAR FAINALI KOMBE LA TFF…YAIPIGA 2-1 JKT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top