• HABARI MPYA

    Sunday, April 01, 2018

    NGORONGORO NA DRC KATIKA PICHA JANA UWANJA WA TAIFA

    Winga machachari wa timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes, Said Mussa 'Ronaldo' akienda chini baada ya kusukumwa na beki wa Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo (DRC),Tshimanga Ramazani katika mchezo wa kwanza kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika nchini Niger mwakani uliomalizikika kwa sare ya 0-0    
    Kipa wa DRC, Mobaelwa Salum akichupia mpira kudaka mbele ya mshambuliaji wa Tanzania, Abdul Suleiman


    Kiungo wa Tanzania, Asad Juma Ali akijaribu kumpita beki wa DRC, Mangindula Henock   


    Winga Said Mussa 'Ronaldo' wa Tanzania, akimpita Christian Katalayi wa DRC


    Mshambuliaji Peter Paul wa Tanzania akimpita beki wa DRC, Mangundula Henock 
    Kiungo wa Tanzania, Ally Ng'anzi akituliza mpira kiufundi mbel;e ya mchezaji wa DRC 
    Riffat Msuya wa Tanzania (kulia akiukata mpira kitaalamu pembeni ya Ifasso Ifunga wa DRC

    Mshambuliaji wa DRC, Muleka Jackson akiondoka na mpira mbele ya beki wa Tanzania, Nickson Kibabage
    Kikosi cha Ngorongoro Heroes kabla ya mchezo wa jana 
    Kikosi cha DRC U-20 kabla ya mchezo wa jana Uwanja wa Taifa
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGORONGORO NA DRC KATIKA PICHA JANA UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top