• HABARI MPYA

  Sunday, April 01, 2018

  NGOMA HAYUPO HATA BENCHI LEO SINGIDA…CHIRWA NA AJIB KUONGOZA SAFU YA USHAMBULIAJI NAMFUA

  Na Prince Akbar, SINGIDA
  MSHAMBULIAJI Mzimbabwe wa Yanga SC, Donald Ngoma hayumo kabisa kwenye programu ya mchezo wa leo wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Singida United.
  Yanga wanateremka Uwanja wa Namfua mjini Singida kumenyana na wenyeji, SIngida katika Robo Fainali ya mwisho ya ASFC kutafuta njia ya kuzifuata Stand United, JKT Tanzania na Mtibwa Sugar.   
  Na kuelekea mchezo huo baadaye kidogo,  kocha Mzambia George Lwandamina ametaja kikosi chake bila kumjumuisha Ngoma, majeruhi wa tangu Novemba mwaka jana aliyetarajiwa kurudi uwanjani leo baada ya kufanya mazoezi wiki yote hii.
  Donald Ngoma hayumo kabisa kwenye programu ya leo dhidi ya Singida United

  Leo Lwandamina amewaanzisha Mzambia mwenzake, Obrey Chirwa na wazawa Pius Buswita, Yussuf Mhilu na Ibrahim Ajib katika safu ya ushambuliaji.
  Ukuta wa Yanga leo utaundwa na kipa Mcameroon, Youthe Rostand atakayelindwa na mabeki Juma Abdul kulia, Gardiel Michael kushoto, Andrew Vincent ‘Dante’ na Kelvin Yondan katikati, wakati viungo watakuwa ni Said Juma ‘Makapu’ na Papy Kabamba Tshishimbi.  
  Kikosi kamili cha Yanga leo ni; Youthe Rostand, Juma Abdul, Gardiel Michael, Andrew Vincent, Kelvin Yondan, Said Juma ‘Makapu’, Yussuf Mhilu, Papy Kabamba Tshishimbi, Obrey Chirwa, Pius Buswita na Ibrahim Ajib.
  Benchi; Ramadhan Kabwili, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji Mngwali, Abdallah Shaibu, Raphael Daudi, Juma Mahadhi na Emmanuel Martin. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGOMA HAYUPO HATA BENCHI LEO SINGIDA…CHIRWA NA AJIB KUONGOZA SAFU YA USHAMBULIAJI NAMFUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top