• HABARI MPYA

  Tuesday, April 03, 2018

  MSUVA AWASUMBUA ILE MBAYA, LAKINI JADIDA YAAMBULIA SARE 0-0 BERKANE LIGI YA MOROCOO

  Na Mwandishi Wetu, BERKANE
  WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana amecheza kwa dakika 78 timu yake, Difaa Hassan El-Jadidi ikipata sare ya ugenini ya 0-0 na RSB Berkane katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola Pro Uwanja wa Manispaa ya Berkane.
  Msuva alicheza vizuri mno jana na kuwasumbua mabeki wa Renaissance Sportive De Berkane kwa chenga na mbio zake kiasi cha kujikiuta anachezewa rafu mara kwa mara.
  Lakini winga huyo wa zamani wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam na mfungaji bora wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara akashindwa kufunga tu jana mara mbili akipiga nje akiwa katika nafasi nzuri.  
  Simon Msuva akimiliki mpira mbele ya beki wa RSB Berkane jana Uwanja wa Manispaa ya Berkane

  Matokeo ya mechi ya jana yanayoiongezea pointi moja Difaa Hassan El-Jadidi, yanaipandisha kwa nafasi mbili hadi ya tatu, wakifikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 23, wakiwa juu ya Raja Casablanca kwa wastani wa mabao tu, nao wakoiwa na pointi 36 lakini za mechi 22.
  Ittihad Tanger ndiyo inaongoza Ligi ya Morocco kwa pointi zake 44 za mechi 23, ikifuatiwa na Hassania Agadir yenye pointi 40 za mechi 23 pia.
  Kikosi cha Difaa Hassan El- Jadidi jana kilikuwa; Aziz El Qinani, Mohamed Hamami, Youssef Aguerdoum El Idrissi, Bakary N'diaye, Marouane Hadhoudi, Fabrice Ngah, Anouar Jayid, Ayoub Nanah/Lhoucein Khoukhouch dk80, Simon Msuva/Adil El Hasnaoui dk78, Hamid Ahadad na Hamza Sanhaji/Bilal El Magri dk78.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA AWASUMBUA ILE MBAYA, LAKINI JADIDA YAAMBULIA SARE 0-0 BERKANE LIGI YA MOROCOO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top