• HABARI MPYA

  Tuesday, April 03, 2018

  SAMATTA AFIKISHA MECHI 80 GENK YAPIGWA 1-0 KWA PENALTI DAKIKA YA MWISHO KABISA UGENINI

  Na Mwandishi Wetu, BRUGGE
  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amefikisha mechi 80 za kuichezea KRC Genk ikichapwa bao 1-0 na Club Brugge katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Jan Breydel mjini Brugge
  Na Genk walikaribia kupata sare ya ugenini kama si bao la penalty la dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kutimia kwa dakika 90 za kawaida la Myahudi Lior Refaelov.
  Samatta jana kwa mara ya kwanza tangu apone mwezi uliopita maumivu ya goti aliyoyapata Novemba mwaka jana alicheza kwa dakika zote 90 na aliisimbua mno ngome ya Club Brugge. 
  Samatta jana amecheza mechi ya 80 tangu alipojiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 
  Na katika mechi hizo, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mashindano yote.
  Kikosi cha Club Brugge vilikuwa: Vermeer, Wesley/Dennis dk64, Diaby/Refaelov dk64, Mitrovic, Limbombe, Vanaken, Cools, Denswil, Vormer, Nakamba na Mechele.
  KRC Genk: Vukovic, Uronen, Colley, Aidoo, Mata, Wouters, Seck, Malinovskyi, Pozuelo/Buffel dk82, Trossard/Ndongala dk76 na Samatta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AFIKISHA MECHI 80 GENK YAPIGWA 1-0 KWA PENALTI DAKIKA YA MWISHO KABISA UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top