• HABARI MPYA

  Tuesday, April 03, 2018

  JUPP HEYNCKES ASEMA LEWANDOWSKI HAENDI REAL MADRID NG'O

  KOCHA wa Bayern Munich, Jupp Heynckes amefunga milango ya kutokea ya mshambuliaji Robert Lewandowski, akisistiza kwamba Real Madrid haina nafasi ya kumsajili mshambuliaji huyo.
  Mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland amekuwa akihusishwa na kuhamia Jiji Kuu la Hispania mwishoni mwa msimu, lakini kocha mkuu wa Bayern amezuia mazungumzo yote ya uhamisho wake.
  "[Mwenyekiti] Karl-Heinz Rummenigge tayari amesema hili: na Robert, Real Madrid hawana nafasi kabisa,"aliwaambia Waandishi wa Habari katika mkutano.

  Robert Lewandowski hataondoka kwenda Bayern Munich msimu ujao, amesema Jupp Heynckes PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 72 bado hajawa na maamuzi juu ya mustakabali wa Franck Ribery na Arjen Robben katika klabu ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu.
  Heynckes amesema: "Nina maoni yangu kwa Ribery na Robben. Lakini sitayasema kwa sasa,"alisema na kuongeza. "Klabu itajua wao ni nani na itaamua kulingana na kazi yao uwanjani,". 
  Kocha huyo wa Bayern Munich aliyasema hayo jana kuelekea mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Sevilla leo.
  Mjerumani huyo aliwaambia Waandshi wa Habari kwamba 'anachotaka ni ushindi tu' dhidi ya wapinzani kutoka Hispania Jumanne, ili kwenda kumalizia vizuri mchezo wa marudiano Uwanja wa Allianz Arena.
  "Nazungumzia matokeo ya jumla, nataka ushindi. Lazima tuingie kwenye mechi kwa fikra za kushinda. Sare ya bila mabao inadanganya, kama ambavyo Manchester United walivyotolewa,".
  Kuhusu timu, Heynckes amesema: "Vidal amefanya mazoezi tena na ninahisi atakuwepo (leo). Juan Bernat pia yuko fiti tena,"..
  Mechi ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa leo, mabingwa watetezi, Real Madrid watakuwa wageni wa Juventus mjini Turin - wakati kesho Barcelona watakuwa wenyeji wa Roma na Liverpool wataikaribisha Manchester City katika mechi ya mahasimu wa Ligi Kuu England.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JUPP HEYNCKES ASEMA LEWANDOWSKI HAENDI REAL MADRID NG'O Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top