• HABARI MPYA

  Friday, April 13, 2018

  LIVERPOOL NA ROMA, REAL MADRID NA BAYERN MUNICH NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA

  TIMU ya Liverpool itakutana na Roma ya Italia katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuelekea kutwaa taji la kwanza la michuano hiyo baada ya miaka 11. 
  Kikosi cha Jurgen Klopp kitawakaribisha wababe wa Serie A Uwanja wa Anfield katika Nusu Fainali ya kwanza Aprili 24 au 25, kabla ya kusafiri kwa mchezo wa marudiano Uwanja wa Olimpico Mei 1 au 2.  
  Real Madrid itaanzia nyumbani dhidi ya Bayern Munich katika Nusu Fainali nyingine kali ya michuano hiyo kabla ya kusafiri kwa mchezo wa marudiano Ujerumani.
  Liverpool imefika Nusu Fainali baada ya kuwatoa vinara wa Ligi Kuu ya England Manchester City kwa jumla ya mabao 5-1, ikishinda 3-0 Anfield na 2-1 Etihad.
  Fainali ya michuano hiyo itafanyika Uwanja wa NSC Olimpiyskiy mjini Kiev, Ukraine Jumamosi ya Mei 26.  

  Liverpool itakutana na Roma ya Italia katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
   PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL NA ROMA, REAL MADRID NA BAYERN MUNICH NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top