• HABARI MPYA

    Friday, April 13, 2018

    ARSENAL YAPEWA ATLETICO MADRID NUSU FAINALI EUROPA LEAGUE

    Arsenal ya England itamenyana na Atletico Madrid ya Hispania katika Nusu Fainali ya michuano ya Europa League PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

    TAREHE ZA MECHI 

    Aprili 26 
    Arsenal v Atletico Madrid 
    Marseille v Red Bull Salzburg
    Mei 3 
    Atletico Madrid v Arsenal
    Red Bull Salzburg v Marseille 
    Arsenal imepangwa kama timu ya nyumbani katika droo ya Nusu Fainali iliyofanyika leo, maana yake wataanzia nyumbani Uwanja wa Emirates.
    Mechi ya kwanza itachezwa Aprili 26 Emirates, wakati marudiano yatafuatia Uwanja wa Wanda Metropolitano Mei 3.
    Mechi hizo mbili dhidi ya Atletico Madrid zitafanyika katikati ya mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Manchester United.
    Na hiyo itakuwa mechi ya kwanza ya ushindani kuwakutanisha Wenger na bosi wa Atletico, Diego Simeone kwa mara ya kwanza kama makocha. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YAPEWA ATLETICO MADRID NUSU FAINALI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top