• HABARI MPYA

  Friday, April 13, 2018

  OKWI AKARIBIA KUTWAA KIATU CHA KWANZA CHA DHAHABU LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Mganda wa Simba SC, Emmanuel Okwi anakaribia kabisa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mara ya kwanza katika historia yake ya kucheza nchini.
  Okwi amecheza na kushinda mataji ya Ligi Kuu akiwa n azote, Simba na Yanga, lakini hajaweza kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu tangu awasili kwa mara ya kwanza nchini mwaka 2010 akitokea SC Villa ya kwao, Kampala.
  Lakini katika msimu wake wa kwanza tangu arejee Simba kwa mara ya pili tangu aondoke mwaka 2015, Okwi yu jirani mno na kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu.
  Okwi anaongoza orodha ya wafungaji bora wa Ligi Kuu kwa mabao yake 18, akifuatiwa na mshambuliaji mwenzake wa Simba, John Raphael Bocco ambaye ni Nahodha mwenye mabao 13, mbele ya mshambuliaji wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa mwenye mabao 12
  Emmanuel Okwi anakaribia kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu 

  Wengine kwenye orodha hiyo ni Eliud Ambokile wa Mbeya City mwenye mabao 10, Habib Kiyombo wa Mbao FC na Mohammed Rashid wa Tanzania Prisons wenye mabao tisa kila mmoja, Asante Kwasi wa Simba SC mwenye mabao nane sawa na Marcel Kaheza wa Maji Maji ya Songea.
  Wengine waliomo kwenye mbio hizo ni Ibrahim Ajib wa Yanga, Shiza Ramadhani Kichuya wa Simba na Paul Nonga wa Mwadui FC wenye mabao saba kila mmoja.
  Wakati Ligi Kuu ikiwa inaelekea ukingoni, Wekundu hao wa Msimbazi wanaongoza kwa pointi zao 55 baada ya kucheza mechi 23, moja zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 47 katika nafasi ya pili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OKWI AKARIBIA KUTWAA KIATU CHA KWANZA CHA DHAHABU LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top