• HABARI MPYA

    Monday, January 22, 2018

    VAN PERSIE AREJEA FEYENOORD BAADA YA MIAKA 14

    Robin van Persie amerejea Feyenoord miaka 14 tangu aondoke kuhamia Arsenal PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    ROBIN VAN PERSIE AREJEA FEYENOORD 

    Robin van Persie amerejea klabu yake ya zamani baada ya kucheza England na Uturuki. Mholanzi huyo aliibukia klabu ya Excelsior kabla ya kujiunga na timu ya vijana ya Feyenoord mwaka 2001. Alifunga mabao 22 katika mechi 78 za Feyenoord kabla ya kunyakuliwa na Arsenal mwaka 2004. Ametwaa mataji ya Kombe la UEFA, sasa linajulikana kama Europa League katika msimu wake wa kwanza mjini Rotterdam.
    MSHAMBULIAJI Robin van Persie amekamilisha uhamisho wake kurejea klabu yake ya ujanani, Feyenoord — miaka 14 tangu aondoke Uholanzi kwenda kujiunga Arsenal. 
    Mshambuliaji huyo Mholanzi alianzia soka katika klabu hiyo, akiibukia kwenye akademi, kabla ya kwenda kufunga mabao 226 kwenye klabu za Arsenal, Manchester United za England na Fenerbahce ya Uturuki.
    Lakini alirejea Jumatatu, akisaini mkataba wa miezi 18 baada ya Fenerbahce kukubali kumuachia aondoke kama mchezaji huru mwezi huu. 
    Baada ya kushindwa kung'ara nchini Uturuki, Van Persie alikubali kurejea nyumbani Ijumaa alipowasili na leo kukamilisha uhamisho wake.
    Baada ya kurejea, Van Persie sasa atakuwa anavaa jezi namba 32 msimu huu, akirejea kwenye namba yake ya kwanza aliyovaa wakati anaibuka mwaka 2002. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VAN PERSIE AREJEA FEYENOORD BAADA YA MIAKA 14 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top