• HABARI MPYA

    Monday, January 29, 2018

    AZAM NA YANGA WAWAFUATA ‘WASIOJULIKANA’ KOMBE LA SHIRIKISHO MORO NA MBEYA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KUFUATIA  kukamilishwa kwa mechi za duru la kwanza la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kalenda ya soka ya Tanzania sasa inahamia kwenye michuano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), ijulikanayo kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa mechi ya hatua ya 32 Bora katikati ya wiki. 
    Vigogo Azam FC na Yanga SC wote wanasafiri kwenda mikoani kumenyana na timu za Ihefu FC na Shupavu FC katika hatua ya 32 Bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).
    Yanga SC wanakwenda Mbeya kuifuata Ihefu, mechi itakayopigwa Uwanja wa Sokoine mjini humo, wakati Azam FC watakwenda Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kumenyana na Shupavu FC.  
    Shaaban Iddi Chilunda (kulia) anatarajiwa kuendelea kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Azam FC
    Green Warriors iliyowatoa mabingwa watetezi, Simba SC itaendelea kucheza nyumbani mjini Dar es Salaam itakapowakaribisha Singida United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
    Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi utahodhi mechi mbili mfululizo za wenyeji, Kariakoo United dhidi ya washindi wa pili wa msimu uliopita, Mbao FC ya Mwanza na Maji Maji Rangers dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro. 
    Maji Maji wataikaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Njombe Mji FC wataikaribisha Rhino Rangers Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe, Kiluvia United wataikaribisha JKT Oljoro Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Ndanda FC watakuwa wenyeji wa Biashara United ya Mara Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
    Mechi nyingine; Pamba SC wataikaribisha Stand United Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Polisi Tanzania watakuwa wenyeji wa Friends Rangers Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, JKT Tanzania watakuwa wenyeji wa Polisi Dar es Salaam na Mwadui FC wataikaribisha Dodoma FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga. 
    Tanzania Prisons wataikaribisha Burkina Faso Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wakati Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Buseresere FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. 
    Mchezo kati ya KMC ya kocha Freddy Felix Minziro wa Toto Africans ya Mwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam umeahirishwa hadi Februari 7 wakati mechi nyingine zite zinatarajiwa kucheza siku mbili mfululizo, Januari 31 na Februari 1, mwaka huu.
    Green Warriors waliowatoa mabingwa Simba, watakuwa wenyeji wa Singida United

    MECHI ZOTE HATUA YA 32 BORA
    JANUARI 30, 2018 
    IHEFU VS YANGA –MBEYA 
    JKT TZ VS POLISI DAR
    POLISI TZ VS FRIEND RANGERS 
    SHUPAVU FC VS AZAM FC
    NDANDA VS BIASHARA
    KARIAKOO LINDI VS MBAO
    KAGERA SUGAR VS BUSERESERE
    JANUARI 31, 2018
    MAJIMAJI FC VS RUVU 
    TZ PRISONS VS BURKINA
    KILUVYA VS JKT OLJORO
    GREEN WARRS VS SINGIDA UNITED
    PAMBA VS STAND UNITED 
    NJOMBE MJI VS RHINO RANGERS 
    JANUARI 7, 2018
    KMC VS TOTO AFRICANS
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM NA YANGA WAWAFUATA ‘WASIOJULIKANA’ KOMBE LA SHIRIKISHO MORO NA MBEYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top