• HABARI MPYA

    Wednesday, January 31, 2018

    TFF YAJISAFISHA MADAI YA KUTOZILIPA TIMU FEDHA ZA UDHAMINI AZAM SPORTS FEDERATION CUP

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesikitishwa na kauli iliyotolewa na golikipa wa timu ya Shupavu ya Morogoro Halifa Mgwira baada ya kumalizika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho la Azam ASFC dhidi ya Azam FC iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro. 
    Wakati akifanyiwa mahojiano Mgwira alizungumza maneno yanayoashiria kuwa wamefungwa kwasababu TFF haijawapa pesa ambazo wanazitumia kwaajili ya chakula. 
    Utaratibu wa TFF ni kuzipatia fedha timu kabla ya kucheza mechi zao utaratibu ambao umefanyika kwa Shupavu waliolipwa fedha zao jana ikiwemo na TFF kuwaongeza fedha ya ziada mara mbili zaidi kama yalivyokuwa maombi yao. 
    TFF inafanya utaratibu wa kumtaka Mgwira kuthibitisha madai yake na endapo atashindwa kuthibitisha ataadhibiwa kwa mujibu wa kanuni.
    TFF inasisitiza kwa wanafamilia wa mpira wa miguu kufuata taratibu katika kuwasilisha malalamiko yao kwa kuwa taratibu ziko wazi.
    Wakati huo huo: Viongozi watatu wa juu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF watahudhuria mkutano mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF utakaofanyika Februari 2, 2018 nchini Morocco.
    Mbali na Rais wa TFF Ndugu Wallace Karia wengine watakaohudhuria mkutano huo ni Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAJISAFISHA MADAI YA KUTOZILIPA TIMU FEDHA ZA UDHAMINI AZAM SPORTS FEDERATION CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top