• HABARI MPYA

    Wednesday, January 31, 2018

    MTIBWA SUGAR, PRISONS, MAJI MAJI NAZO ZATINGA 16 BORA AZAM SPORTS FEDERATION

    Na Mwandishi Wetu, LINDI
    TIMU ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kwenda hatua ya 16 Bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Maji Maji Rangers Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
    Mabao ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa leo yamefungwa na mshambuliaji Kevin Sabato Kongwe yote mawili na yote kwa mipira ya adhabu, la kwanza dakika ya 36 baada ya Haruna Chanongo kuangushwa na la pili dakika ya 46 baada ya Salum Kihimbwa kuangushwa.
    Maji Maji walipata bao la kufutia machozi dakika ya 84 kwa penalti, lililofungwa na Peter Pole kwa bada ya Issa Kadia Mwanga wa Mtibwa Sugar kuunawa mpira kwenye boksi.
    Mechi nyingine za leo Tanzania Prisons imesonga mbele kwa ushindi wa penalti 5-4 baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Burkina Faso FC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya leo na Maji Maji ya Songea imeshinda 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani.
    Nayo Njombe Mji FC imeshinda kwa penalti 4-1 baada ya sare ya 2-2 na Rhino Rangers Uwanja wa Saba Saba, Njombe, Stand United imeichapa Pamba FC 2-0 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na Kiluvya United ya kocha Yahya Issa imeichapa 2-0 JKT Oljoro Uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani.
    Singida United wameshinda kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Green Warriors Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, wakati mechi kati ya KMC na Toto Africans imesogezwa mbele hadi Februari 7, mwaka huu.
    Ikumbukwe katika mechi za jana, Azam FC iliwatoa wenyeji Shupavu FC kuwa kuwachapa mabao 5-0 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Yanga iliwatoa wenyeji Ihefu kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Ndanda FC ilishinda kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 1-1 na Biashara United ya Mara Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
    Mechi nyingine ASFC; Mbao FC ilisshinda 1-0 dhidi ya wenyeji Kariakoo United Uwanja wa Ilulu, Lindi, Dodoma FC ilishinda 2-1 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga, Buseresere FC  ilishinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Polisi Tanzania iliifunga Friends Rangers 2-1 Uwanja wa Ushirika mjini Moshi na JKT Tanzania iliifunga Polisi Dar 1-0 mjini Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIBWA SUGAR, PRISONS, MAJI MAJI NAZO ZATINGA 16 BORA AZAM SPORTS FEDERATION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top