• HABARI MPYA

  Tuesday, January 23, 2018

  UGANDA YAONDOKA NA PONTI MOJA TU CHAN 2018 MOROCCO

  TIMU za Uganda na Ivory Coast jana zimeambulia pointi moja moja kwenye michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya sare ya 0-0 baina yao katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi B mjini Marrakech, Morocco.
  Na baada ya kufungwa mechi zao mbili mbili za kwanza za kundi hilo, Uganda na Ivory Coast zinapakia mizigo pamoja na pointi hizo moja moja kurejea Kampala na Abidjan zikiiacha CHAN ikiingia katika hatua ya mtoano.
  Lakini jana timu zote zilionyesha kiwango kizuri ukilinganisha na zilivyocheza kwenye mechi zake mbili za kwanza.
  Katika mchezo mwingine wa kundi hilo uliofanyika mjini Casablanca, Zambia walitoka nyuma na kupata sare ya 1-1 na Namibia.
  Kwa matokeo hayo, Zambia inamaliza kileleni mwa Kundi kwa wastani wake mzuri wa mabao baada ya kulingana kwa pointi na Namibia, saba kila mmoja.
  CHAN inaendelea leo kwa mechi za mwisho za Kundi C, ambalo ndilo gumu zaidi, Equatorial Guinea wakimenyana na Nigeria Uwanja wa Agadir na Rwanda na Libya Uwanja wa Ibn Batouta, mechi zote zitaanza Saa 4:00 usiku.
  Kutoka Kundi A, Morocco na Sudan zimefuzu Robo Fainali tayari, kama ilivyo kwa Zambia na Namibia kutoka Kundi B na Kongo pekee kwa Kundi D.
  Kundi C Nigeria na Rwanda zinafungana kwa pointi nne kila moja zikifuatiwa na Libya yenye pointi tatu, wakati Equatorial Guinea ambayo haina pointi inashika mkia.
  Kundi D Kongo imefuzu tayari kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Angola yenye poini nne ambayo kesho itacheza na Kongo, wakati Burkina Faso yenye pointi moja itamaliza na Cameroon ambayo haina kitu.  
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UGANDA YAONDOKA NA PONTI MOJA TU CHAN 2018 MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top