• HABARI MPYA

    Wednesday, February 25, 2026

    YANGA YAIMIMINIA MABAO 5-0 JKT TANZANIA MWENGE


    MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
    Mabao ya Yanga SC yamefungwa na beki Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ dakika ya saba, mshambuliaji Muangola Laurindo Dilson Maria Aurelio ‘Depu’ dakika ya 60, kiungo Mudathir Yahya Abbas dakika ya 63, mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Mpumelelo Dube dakika ya 84 na kiungo Shekhan Ibrahim Khamis dakika ya 89.
    Kwa ushindi huo, Yanga wanafikisha pointi 28 katika mchezo wa 10 na kupanda kileleni ikiizidi tu wastani wa mabao JKT Tanzania, ambayo pia imecheza mechi saba zaidi. 

    Mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo Dube ndiye Mchezaji Bora wa Mechi leo
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YAIMIMINIA MABAO 5-0 JKT TANZANIA MWENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top