• HABARI MPYA

  Monday, January 22, 2018

  MOROCCO YAMALIZIA KILELENI CHAN, UGANDA WAKAMLISHA RATIBA LEO

  KIUNGO Achraf Bencharki alikosa penalti jana dakika ya tano baada ya kuanza kipindi cha pili, Sudan ikitoka sare ya bila mabao na wenyeji Morocco katika mchezo wa kukamilisha mechi za Kundi A Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mjini Casablanca.
  Sare hiyo inaihakikishia Morocco kumaliza kileleni mwa kundi hilo, ikifuatiwa na Sudan katika nafasi ya pili, Guinea wa tatu na Mauritania wameshika mkia.
  Kocha wa Morocco, Jamal Sellami alifanya mabadiliko kikosini mwake jana akimuanzisha Achraf Bencharki na mchezaji mwenzake wa Wydad Athletic, Walid El Karti lakini wenyeji hao wakaihis akukosa mabao ya wazi.
  Mechi nyingine ya kukamilisha michezo ya Kundi A jana, Guinea iliifunga Mauritania 1-0 mjini  Marrakech.
  Michuano ya CHAN inaendelea leo kwa mechi za Kundi B, Namibia na Zambia Uwanja wa Mohamed na Uganda na Ivory Coast Uwanja wa Marrakech, zote zikianza Saa 4:00 usiku.
  Ikumbukwe tayari Zambia na Namibia zimefuzu Robo Fainali sawa na Morocco na Sudan kwa Kundi A, wakati timu nyingine iliyojihakikishia tiketi ya Nane Bora ni Kongo kutoka Kundi D.
  Kundi C, Nigeria yenye pointi nne sawa na Rwanda na Libya yenye pointi tatu kuelekea mechi za mwisho za makundi, zote zina nafasi ya kwenda Robo Fainali.    
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOROCCO YAMALIZIA KILELENI CHAN, UGANDA WAKAMLISHA RATIBA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top