• HABARI MPYA

    Thursday, April 23, 2026

    MWALIMU 'GOMEZ' AIPELEKA SIMBA SC NUSU FAINALI KOMBE LA MUUNGANO


    TIMU ya Simba SC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Muungano baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mafunzo usiku hui Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Bao pekee la Simba SC katika mchezo wa leo limefungwa na mshambuliaji wake tegemeo kwa sasa, Suleiman Abdallah Mwalimu ‘Gomez’ dakika ya 54.
    Simba SC sasa itakutana na Mlandege FC katika Nusu Fainali Jumapili, baada ya mabingwa watetezi, Yanga kucheza na Azam FC katika Nusu Fainali ya kwanza Jumamosi, mechi zote zikianza kuanzia Saa 2:15 usiku hapo hapo Uwanja wa New Amaan Complex 
    Mlandege FC imetinga Nusu Fainali baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars jioni ya leo hapo hapo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Mabao ya Mlandege yamefungwa na Omar Juma’Samatta’ dakika ya 28 na Mussan Hassan ‘Mbappe’ dakika ya 45’+1, baada ya Mishamo Daudi kuanza kuifungia Singida Black Stars dakika ya tisa.
    Wakati Yanga iliitoa Muembe Makumbi City FC kwa kuichapa mabao 4-0 juzi, Azam FC iliitupa nje KVZ FC KWA kuichapa mabao 2-0 hapo hapo Amaan Complex.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWALIMU 'GOMEZ' AIPELEKA SIMBA SC NUSU FAINALI KOMBE LA MUUNGANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top