• HABARI MPYA

    Monday, January 22, 2018

    GWIJI WA ENGLAND, MTANGAZAJI AFARIKI DUNIA

    GWIJI wa England na mtangazaji mwenye heshima kubwa, Jimmy Armfield amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 82 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani. 
    Pamoja na kuichezea mechi 569 Blackpool enzi zake, Armfield pia alikuwa Nahodha wa England mara 15 katika mechi 43 alizochezea Simba Watatu. 
    Baada ya kuwa kocha wa timu za Leeds na Bolton, Armfield akahamia kwenye utangazaji na kujivunia heshima kubwa akiwa mchambuzi wa BBC Radio 5 Live. 
    Familia yake imethibitisha kifo chake kilichotokea Trinity Hospice mapema asubuhi ya leo. Mungu ampumzishe kwa amani gwiji huyo. Amin.
    Jimmy Armfield akipokea tuzo maalum ya Chama cha Wachezaji wa Kulipwa England (PFA) mwezi Aprili mwaka 2008 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GWIJI WA ENGLAND, MTANGAZAJI AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top