• HABARI MPYA

  Sunday, July 09, 2017

  ZIMBABWE MABINGWA WA KIHISTORIA COSAFA, WAIGONGA 3-1 ZAMBIA

  TIMU ya taifa ya Zimbabwe imetwaa taji la tano la rekodi la Kombe la COSAFA Castle baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Zambia katika fainali iliyofanyika jioni ya leo Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace mjini Rusternburg, jimbo la Kaskazini Magharibi, Afrika Kusini.
  Zimbabwe ndiyo imekuwa timu bora ya mashindano, ikicheza mechi sita ndani ya siku 14 na kufunga mabao mazuri 19.
  Mabao ya Zimbabwe yamefungwa na Knox Mutizwa dakika ya 22, Talent Chawapiwa dakika ya 57 na Ocean Mushure dakika ya 67 wakati la Zambia lilifungwa na Lubinda Mundia dakika ya 39.
  Zimbabwe sasa ndiyo inaongoza kutwaa Kombe la COSAFA, ikiwa imebeba taji hilo mara tano, mara moja zaidi ya Zambia na Afrika Kusini. 
  Kwa Zambia hii ni mara ya tano inafungwa katika fainali ambayo ni rekodi kwenye michuano hiyo. Nahodha wa Zimbabwe, Ovidy Karuru ameibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa mabao yake sita, moja zaidi ya mchezaji mwenzake, Knox Mutizwa.
  Kwa ushindi huo, Zimbabwe inazawadiwa dola 42,000 na mshindi wa pili dola 21,000, wakati Tanzania iliyomaliza nafasi ya tatu baada ya kuifunga Lesotho kwa penalty 4-2 kufuatia sare ya 0-0 ilizawadiwa dola za Kimarekani 10,000 zaidi ya Sh. Milioni 22 kwa fedha za nyumbani. Lesotho wamepata dola 8,300.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZIMBABWE MABINGWA WA KIHISTORIA COSAFA, WAIGONGA 3-1 ZAMBIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top