• HABARI MPYA

    Sunday, July 09, 2017

    SAID MOHAMMED MDUDA KIPA BORA COSAFA 2017

    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    MTANZANIA Said Mohammed Mduda ndiye kipa bora wa mashindano ya COSAFA Castle 2017 licha ya kudaka mechi moja tu.
    Mchezaji huyo wa Mtibwa Sugar ya Morogoro amemzidi kipa mwenzake wa Tanzania, Aishi Manula aliyedaka mechi zote tano za awali za Taifa Stars katika COSAFA.
    Kipa bora COSAFA 2017 kwa kudaka mechi moja tu
    Manula alidaka Stars ikishinda 2-0 dhidi ya Malawi, ikitoa sare ya 0-0 na Angola, 1-1 na Mauritius, ikishinda 1-0 dhidi ya Afrika Kusini na katika kipigo cha 4-2 dhidi ya Lesotho, lakini haikumsaidia kuonekana bora mbele ya jopo la wataalamu wa COSAFA.
    Lakini Mduda baada ya kudaka vizuri ndani ya dakika 90 tu dhidi ya LesotHo na kwenda kuiongoza Stars kushinda kwa penalti 4-2 na kushika nafasi ya tatu, amekuwa kipa bora wa mashindano ya 2017.
    Mduda alipangua penalti ya Nahodha wa Mamba, Thapelo Mokhehle kufuatia Sera Motebang kugongesha mwamba wa kulia mkwaju wake na kurudi uwanjani.
    Waliofunga penalti za Lesotho ni Hlompho Kalake na Tsoanelo Koetle wakati Shiza Kichuya aligongesha mwamba wa juu penalti ya kwanza ya Tanzania, kabla ya Nahodha Himid Mao, Simon Msuva, Abdi Banda na Raphael Daudi kumtungua kipa wa Mamba Samuel Ketsekile kuipatia Taifa Stars ushindi mzuri wa 4-2.
    Kutokana na ushindi huo, Tanzania imepata dola za Kimarekani 10,000 zaidi ya Sh. Milioni 22 kwa fedha za nyumbani, wakati Lesotho wamepata dola 8,300.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAID MOHAMMED MDUDA KIPA BORA COSAFA 2017 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top