• HABARI MPYA

  Sunday, July 09, 2017

  WAYNE ROONEY AREJEA EVERTON MIAKA MIWILI, KUTUA TANZANIA WIKI IJAYO


  Amerejea kwenye bluu: Wayne Rooney amejiunga tena na klabu yake ya utotoni kutoka Manchester United 
  PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  MATAJI YA WAYNE ROONEY MAN UNITED 

  LIGI KUU: 2006–07, 2007–08, 2008–09, 2010–11, 2012–13
  KOMBE LA FA: 2015–16
  KOMBE LA LIGI: 2005–06, 2009–10, 2016–17
  NGAO YA JAMII: 2007, 2010, 2011, 2016
  LIGI YA MABINGWA ULAYA: 2007–08
  KOMBE LA UEFA Europa League: 2016–17
  KLABU YA DUNIA: 2008
  MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amejiunga tena na Everton baada ya kuondoka Manchester United kama mchezaji huru, klabu hiyo ya Merseyside imethibitisha leo.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amekamilisha uhamisho wake kurejea Goodison Park baada ya miaka 13 tangu aondoke kuhamia United kwa dau la Pauni Milioni 26.5.
  Everton imethibitisha mkataba huo wa miaka miwili kwa video fupi yenye maneno 'karibu nyumbani Wayne'. Rooney amezungumzia uhamisho huu wa kuvutia na kusema: "Kushinda mataji na Everton inaweza tamu. Ukweli sasa nafikiri klabu inaelekea katika mwelekeo sahihi, kusajili aina aya wachezaji sahihi. Nataka kuwa sehemu ya hili na ni maatumaini sehemu ya tim ya Everton ya mafanikio,".
  Rooney sasa anatarajiwa kuwamo kwenye msafara wa Everton utakaozuru Tanzania wiki ijayo kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya Julai 13, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAYNE ROONEY AREJEA EVERTON MIAKA MIWILI, KUTUA TANZANIA WIKI IJAYO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top