• HABARI MPYA

    Saturday, July 22, 2017

    TENGA AULA TENA CAF, APEWA KAMATI BOSI WAKE BWALYA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chilla Tenga ameteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
    Tenga, aliyewahi pia kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na Mjumbe wa Kamati mbalimbali za CAF awali, atakuwa chini ya Rais Mzambia, Kalusha Bwalya kwenye Kamati hiyo.
    Wote wawili, Rais na Makamu wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya CAF ni wachezaji na Manahodha wa zamani wa nchi zao, Tenga akicheza kama sentahafu na Bwalya ambaye pia ni Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Zambia (FAZ) alikuwa mshambuliaji.
    Leodegar Tenga (kulia) akiwa na Jellah Mtagwa, mchezaji mwenzake wa zamani wa Pan Africans na Taifa Stars 

    Uteuzi huo umefanyika katika Mkutano Mkuu wa CAF Ijumaa mjini Rabat, Morocco ambao pamoja na uundwaji upya wa Kamati mbalimbali, pia ulirekebisha muundo wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na sasa yatakuwa yakifanyika katikati ya mwaka badala ya mwanzoni.
    Mbali na kuzitoa Fainali za AFCON katikati ya mwaka hadi mwanzoni, pia idadi ya timu za kushiriki zinaongezeka hadi 24 kutoka 16.
    Michuano hiyo kuhamishwa kutoka Januari na Februari hadi Juni na Julai kuanzia Fainali za mwaka 2019 nchini Cameroon ni habari njema kwa makocha wa Ligi Kuu ya England na Ulaya kwa ujumla. 
    Makocha wa England na Ulaya kwa ujumla wamekuwa wakiichukia michuano ya AFCON kwa sababu hufanyika kipindi ambacho Ligi zao zimeshika kasi na wachezaji wao tegemeo wa Kiafrika hulazimika kurejea nyumbani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TENGA AULA TENA CAF, APEWA KAMATI BOSI WAKE BWALYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top