• HABARI MPYA

    Wednesday, July 12, 2017

    SIMBA NA YANGA AGOSTI 23 NGAO YA JAMII TAIFA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WATANI wa jadi, Simba na Yanga watakutana Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria kupenuliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amewaambia Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam kwamba, Ligi Kuu yenyewe itaanza Agosti 26, mwaka huu.
    Mabingwa wa Ligi Kuu, Yanga watakutana na washindi wa Kombe la TFF, maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Agosti 23 katika mchezo wa Jamii na wiki moja baadaye kitimutimu cha Ligi Kuu kitaanza.
    Mechi za Ufunguzi Agosti 26 zitazikutanisha Ndanda na Azam FC Uwanja wa Nangwanea Sijaona, Mtwara, Simba SC na Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mwadui FC na Singida United Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga, Mtibwa Sugar na Stand United Uwanja wa Manungu,Turiani, Morogoro, Kagera Sugar na Mbao FC Uwanja wa Kaitaba Bukoba, Nombe Mji na Tanzania Prisons na Mbeya City dhidi ya Majimaji Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
    Mabingwa watetezi, Yanga wataanza kutetea taji lao Jumapili ya Jumapili Agosti 27 kwa kumenyana na Lipuli ya Iringa Uwanja wa Taifa, wakati Oktoba 14 watamenyana na mahasimu wao, Simba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA YANGA AGOSTI 23 NGAO YA JAMII TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top