• HABARI MPYA

  Wednesday, July 12, 2017

  'MIDO' MGHANA JAMES KOTEI AONGEZA MKATABA SIMBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Mghana, James Agyekum Kotei amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Simba SC, kufuatia ule wa awali wa miezi kumalizika.
  Kotei alisaini mkataba huo jana jioni mjini Dar es Salaam mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu, Zacharia Hans Poppe na kumaliza tetesi kwamba alikuwa anataka kuhamia kwa mahasimu, Yanga.
  Mchezaji huyo ambaye Agosti 10 mwaka huu atafikisha umri wa miaka 24, alijiunga na Simba SC Desemba mwaka jana akitokea Al-Oruba ya Oman aliyoanza kuichezea mwaka 2015 akitokea Liberty Professionals ya kwao, Ghana iliyominua mwaka 2010.


  Kiungo Mghana, James Kotei (kushoto) akisaini mkataba na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe (kulia) jana

  Kotei ambaye mwaka 2014 alicheza kwa mkopo BA Stars, aalisajiliwa Simba pamoja na Mghana mwenzake, kipa Daniel Agyei aliyetokea Medeama SC ya kwao pia.
  Lakini taarifa zisizo rasmi zinasema Simba inaachana na mlinda mlango aliuyeng’ara katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka jana akiwa Medeama SC baada ya kumpata kipa namba moja Tanzania, Aishi Manula kutoka Azam FC.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: 'MIDO' MGHANA JAMES KOTEI AONGEZA MKATABA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top