• HABARI MPYA

  Saturday, July 22, 2017

  SAMATTA, ROONEY WAFUNGA GENK NA EVERTON ZATOA SARE 1-1

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  NYOTA ya mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta imeendelea kung’ara barani Ulaya, baada ya leo kuifungia timu yake, Genk katika sare ya 1-1 na Everton ya England katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk, Ubelgiji.
  Nahodha wa Taifa Stars, Samatta aliifungia Genk bao la kusawazisha dakika ya 55 baada ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney kuanza kuifungia Toffees dakika ya 45.
  Mbwana Samatta akishangilia baada ya kuifungia Genk bao la kusawazisha dhidi ya Everton leo 

  Mbwana Samatta akifumua shuti kuifungia bao la kusawazisha Genk leo
  Mbwana Samatta akimtoka beki mpya wa kati wa Everton, Michael Keane leo

  Huo unakuwa mchezo wa 63 kwa Samatta tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana kutoka TP Mazembe ya DRC, akiwa kufunga mabao 24.
  Ikumbukwe katika msimu wake wa kwanza, Samatt alikabidhiwa jezi namba 77, lakini baada ya kazi nzuri, msimu huu amebadilishiwa jezi na kukabidhiwa namba 10.
  Kikosi cha Genk kilikuwa: Jackers, Nastic, Brabec/Seigers dk86, Colley, Khammas, Berge, Malinovskyi/Heynen dk75, Trossard, Buffel/Writers dk72, Benson/Zhegrova dk75 na Samatta/Vanzeir dk62.
  Everton: Pickford/Stekelenburg dk46, Schneiderlin/Connolley dk67, Baines/Barry dk67, Keane, Williams/McCarthy dk73, Ramirez/Mirallas dk46, Rooney/Calvert Lewin dk79, Gueye/Davies dk73, Klaassen/Besic dk73, Dowell/Lookman dk67 na Holgate/Martina dk46.
  Wayne Rooney akiifungia bao la kuongoza Everton leo Uwanja wa Luminus Arena
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA, ROONEY WAFUNGA GENK NA EVERTON ZATOA SARE 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top