• HABARI MPYA

  Saturday, July 22, 2017

  MSUVA MDOGO ATUA MBAO FC MIAKA MIWILI

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  MDOGO wa mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva aitwaye James amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Mbao FC ya Mwanza.
  Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Zephania Njashi ameiambia Bin Zubeiry Sports - Online leo kwamba, Msuva aliyewahi kuchezea timu za vijana za JKT Ruvu, Simba na Yanga, amesaini mkataba huo baada ya kufuzu majaribio katika mchujo maalum ulioandaliwa na timu hiyo.
  Njashi amesema kocha Mrundi, Etienne Ndayiragije amevutiwa na kipaji cha mshambuliaji huyo chipukizi mwenye kipaji cha kufunga mabao baada ya kumjaribu mazoezini kwa wiki moja.  
  James Msuva kushoto baada ya kusaini mkataba wa kujiunga na Mbao FC ya Mwanza
  "Tumemsajili Msuva kutokana na uwezo wake na siyo  sababu labda ni mdogo wa Simon Msuva, hapana. James alikuja Mwanza na akacheza mwalimu akamuona na akaona anatufaa ndiyo maana tumemchukua na kumpa mkataba wa miaka miwili,"amesema Njashi.
  Mbao FC imeendesha mchujo maalum wa kuangalia vijana wa kusajili ili kuunda kikosi cha msimu ujao, kufuatia wachezaji wake kadhaa nyota kuchukliwa na timu za Dar es Salaam baada ya msimu wake mmoja tu wa kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara tangu ipande.
  Walioondoka ni pamoja na kipa Emmanuel Mseja na beki Jamal Mwambeleko waliokwenda Simba, kipa Benedict Haule na kiungo Salmin Hoza waliokwenda Azam na kiungo Pius Buswita aliyekwenda Yanga. 
  Wakati huo huo: Mbao FC itacheza mechi ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Sony Sugar ya Kenya Julai 25, mwaka huu Rorya mkoani Mara.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA MDOGO ATUA MBAO FC MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top