• HABARI MPYA

  Sunday, July 09, 2017

  LUKAKU AKAMILISHA VIPIMO VYA AFYA SAFARI NI MAN UNITED

  MSHAMBULIAJI Mbelgiji, Romelu Lukaku amekamilisha vipimo vya afya kuelekea usajili wake Manchester United kutoka Everton kwa dau la rekodi.
  Lukaku amefanyiwa vipimo vya afya mjini Los Angeles, Marekani jana na kubakisha hatua chache mno kukamilisha uhamisho wake.
  Mapema klabu hiyo ilithibitisha wamekubaliana na Everton ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 75 pamoja na Pauni Milioni 15 zitakazoongezeka kutegeama na kiwango chake Old Trafford, hivyo kumfanya awe mchezaji ghali kuliko  Paul Pogba aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 89.
  Na baada ya kukamilisha vipimo leo, Lukaku akaposti katika akaunti yake Instagram kuwaambia mashabiki wake juu ya zoezi hilo linavyoendelea.
  Ameposti video kadha, lakini picha ya mwisho mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kuposti ni ameonyesha alama ya dole gumba ikiwa na maelezo; 'Finito!'.

  Romelu Lukaku ameposti picha akiwa anaonysha alama hii ya dole gumba kuashiria mambo safi huku ameandika maelezo; 'Finito!' PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUKAKU AKAMILISHA VIPIMO VYA AFYA SAFARI NI MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top