• HABARI MPYA

  Thursday, July 20, 2017

  KIPA NAMBA MOJA GHANA ATUA MARITZBURG UNITED

  KLABU ya Maritzburg United ya Afrika Kusini imekamilisha uhamisho wa kipa wa kimataifa wa Ghana, Richard Ofori.
  Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 23, ambaye ni chaguo la kwanza kwa sasa Black Stars, amewasili KwaZulu-Natal baada ya kuwa amehusishwa na kuhamia Mamelodi Sundowns wiki za karibuni.
  “MUFC inathibitisha kumsajili kipa wa Ghana kwa mkataba wa miaka mitatu unaoweza kuongezeka,” imesema taarifa ya United.
  Kipa namba moja wa Ghana, Richard Ofori amejiunga na Maritzburg United ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu

  Anakuja kuchukua nafasi ya kipa wa kimataifa wa Namibia, Virgil Vries ambaye aliondoka klabuni mwishoni mwa msimu uliopita.
  Ofori amedaka mechi zote tatu za timu ya taifa tangu kurejea kwa kocha Kwesi Appiah, ya karibuni ikiwa ni ya kipigo cha 2-1 ugenini kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mrekani.
  Pia alicheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon mapema mwaka huu, akiibuka katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Ghana ikifungwa 1-0 na Burkina Faso.
  Oforo aliisaidia WA All Stars kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Ghana mwaka 2016, kabla ya kushinda tuzo ya Kipa Bora wa Msimu huo nchini humo.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPA NAMBA MOJA GHANA ATUA MARITZBURG UNITED Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top