• HABARI MPYA

  Thursday, July 20, 2017

  KILICHO NYUMA YA PAZIA JUU YA KUONDOKA KWA NEYMAR BARCELONA...

  HUO utakuwa uhamisho wa kutikisa soka ya Ulaya tangu Real Madrid walipomnasa Luis Figo mwaka 2000, na kwa mara nyingine Barcelona watakuwa waathirika.
  Neymar anaelekea kuondoka kwenye kivuli cha Lionel Messi na kuhamishia ufalme wake Uwanja wa Parc des Princes, ni mchezaji ambay eWakatalunya walitarajiwa atawapiku wote Ulaya wakati wanamnunua mwaka 2013.
  Lakini wapo hatarini kumpoteza baada ya miaka minne tu, kwa ada ambayo itavunja rekodi ya duinia.
  "Sifikirii kama hilo litatokea,"alisema Katibu wa Ufundi wa Barcelona, Robert Fernandez Jumatatu alipoulizwa kuhusu dau la Pauni Milioni 196 za bei ya Neymar.
  Barcelona inaonekana kuchoshwa na tabia za Neymar kupenda anasa kiasi cha kutojali majukumu yake ipasavyo 

  Mwenyekiti wa PSG, Nasser al-Khelaifi anashawishika kwamba anaweza kutimiza ndoto za kutwaa ubingwa wa Ulaya iwapo atamnasa Neymar.
  Ni Neymar aliyeizuia PSG kusonga mbele msimu uliopita kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kung'ara katika ushindi wa jumla wa 6-5 akifunga kwa shuti la hatari la mpira wa adhabu, kwa penalti na kusaidia kupatikana kwa bao la ushindi dakika ya 95.
  Inasemekana huo ndiyo ulikuwa usiku ambao alikwenda juu ya Messi kama mchezaji muhimu zaidi Barcelona. Lakini hawakufanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa.
  The Brazilian went partying with F1 driver Lewis Hamilton after Barcelona's win over PSG
  Neymar alikwenda 'kujirusha' na dereva wa F1, Lewis Hamilton baada ya Barcelona kuitoa PSG

  Neymar alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano Barcelona ikichapwa 2-0 Malaga wiki chache baadaye na wakati anakwenda nje akampigia makofi ya kumkejeli mwamuzi wa akiba, jambo ambalo lilimponza kuongezewa adhabu ya mechi moja zadi na akaikosa El Clasico wiki mbili baadaye.
  Barcelona ikaifunga Real Madrid bila yeye shukrani kwake Messi, aliyefunga bao la ushindi dakika ya 92 — jambo ambalo lilimrudishia heshima yake ya Na 1 Nou Camp na kuonyesha ni jinsi itakuwa vigumu kwa Neymar kumpiku. 
  Wakati Barcelona ikimaliza msimu vibaya, Neymar pia akaanza kuhisi atakuwa ananyooshewa vidole vya lawama.
  Alikwenda kujirusha na Lewis Hamilton usiku wa ushindi wa 6-1 dhidi ya PSG. Alipewa ruhusa, lakini siku nne baada ya sherehe yake na dereva Muingreza wa Formula 1 ambaye urafiki wao ulianzia Marekani walipokutaka katika mapumziko ya kabla ya msimu uliopita alikosekana sababu ya maumivu kwenye mchezo ambao Barcelona ilifungwa 2-1 na Deportivo.
  This week, the Brazilian has been with his friends on a luxury yacht in the party capital of Ibiza
  Wiki hii, Mbrazil huyo alikuwa na rafiki zake wakijirusa mjini Ibiza

  Mchezo huo ulichezwa siku ya sherehe ya kuzaliwa kwa dada yake Neymar, Rafaella na iligundulika huo ulikuwa mwaka wa tatu anakosekana kwenye mechi katika tarehe hiyo hiyo ya mwezi huo.
  Kama ilivyokuwa kwa Hamilton, pia akawa  rafiki wa mwimbaji Mcanada, Justin Bieber ambaye walikuwa wanasafiri naye London siku za mapumziko. 
  Na mwishoni mwa msimu katika viwanja vya mazoezi alikorofishana na Kocha Msaidizi wa wakati huo Barcelona, Carles Unzue ambaye alimuonya Neymar kutoishia kama nyota mwingine Mbrazil wa Barca, Ronaldinho ambaye anasa zilifupisha maisha yake ya uwanjani.
  Neymar is unlikely to ever get out of the shadow of superstar Lionel Messi at the Nou Camp
  Neymar anataka kuondoka kwenye kivuli cha Lionel Messi Uwanja wa Nou Camp

  Unzue ameondoka, lakini hisia zimebaki kwamba Neymar anaonekana kama "mchezaji mpenda starehe" na si kiongozi wa timu. 
  Anaonekana zaidi ya mtu mwenye furaha akiwa pamoja na Messi na Luis Suarez kwenye Uwanja wa mazoezi – watatu hao wana umoja sana mazoezini jambo ambalo linawafanya hata kwenye mechi wawe hatari.
  Lakini umoja wao unatarajiwa kutengenishwa na mpango wa mmoja wao, Mbrazil kuhamia Paris. 
  It is believed former Barca coach Carles Unzue warned Neymar not to end up like Ronaldinho
  Kocha Msaidizi wa zamani wa Barca, Carles Unzue alimuomya Neymar kutoisha kama Ronaldinho

  PSG waliibuka ghafla dakika za mwishoni kuipokonya tonge mdomoni Manchester na kocha Pep Guardiola kwwa kumsajili Dani Alaves, kwa sababu walijua kuna kitu cha ziada atawasaidia katika kumpata Neymar.
  Waumini wa Barcelona wanaweza kupuuza habari za Neymar kuondoka kwa sababu za kisoka tu. Anawezaje kucheza mbele ya mashabiki 48,000 tu kila wiki katika Ligi ya Ufaransa badala ya kubaki Clasico mbele ya watu 99,000? Anaweza kutengana na Messi na Suarez ili kuongeza nafasi yake ya kushinda Ballon d'Or? Vipi kama PSG chini ya kocha Unai Emery itarudia mafanikio ya msimu uliopita na Kombe la Ufaransa ndilo taji pekee walilotwaa?
  Wengone hawataamini kuondoka kwake hadi hadi PSG watakapolipa Euro Milioni 222 na Ligi ya Hispania kumruhusu kuondoka – hata kama Barca wanamtaka Marco Veratti wataitaka PSG ilipe kiasi kamili kisha ndipo wajadili biashara nyingine.
  Barcelona are ready to splash some of the £196million on Paris Saint-Germain's Marco Verratti
  Barcelona ipo tayari kutoa Pauni Milioni 196 kwa Paris Saint-Germain kumnunua Marco Verratti

  Mwaka jana tu amesaini mkataba mpya na Barcelona hadi mwaka 2021, lakini wiki hii habari zimebadilika inaelezwa anataka kuondoka. Magazeti ya Hispania Jumatatu yameripoti kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hana furaha na na gazeti moja likiwa limebandika picha za Neymar akiwa yachi ya Mediterranean saa 24 baadaye anajirusha na rafki zake.
  Tovuti ya Goal.com ikaahidi kuibua mahojiano maalum na mchezaji huyo juu ya mustakabali wake, lakini habari za baba yake Neymar kuwa njiani kwenfa Paris kwa mazungumzo asubuhi hii zinaongeza uzito wa ukweli wa yeye kuondoka. 
  Klabu nyingine za Ligi Kuu England zinaendelea kufuatilia sakata hilo kimya kimya ili ikithibitika anauzwa kweli, nazo zijaribu bahati.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KILICHO NYUMA YA PAZIA JUU YA KUONDOKA KWA NEYMAR BARCELONA... Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top