• HABARI MPYA

    Friday, July 21, 2017

    CAF YAIGEUZIA KIBAO ZANZIBAR, YAIPORA UANACHAMA

    SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeiondoa Zanzibar katika orodha ya nchi wanachama wake, miezi minne tu tangu iipe hadhi hiyo.
    Rais wa CAF, Ahmad amesema Zanzibar, ambayo ni sehemu ya Tanzania haikupaswa kuwa mwanachama wa 55 wa CAF mwezi Machi.
    "Walikubaliwa bila kuangalia vizuri sheria ambazo ni wazi," alisema Ahmad. "CAF haiwezi kukubali vyama viwili tofauti kutoka nchi moja.".
    "Utambulisho wa nchi unatokana na kwa mwanachama wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa," aliongeza Mcomoro huyo katika Mkutano Mkuu wa CAF nchini Morocco wiki hii.
    FIFA walikataa kuipa Zanzibar uanachama, baada ya CAF, chini ya Ahmad kuingia madarakani akimuangusha Mcameroon Issa Hayatou na kukikubalia kisiwa hicho cha Afrika Mashariki kuwa mwanachama wake.
    Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini imekuwa ikiendesha shughuli zake za soka yenyewe.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAF YAIGEUZIA KIBAO ZANZIBAR, YAIPORA UANACHAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top