• HABARI MPYA

  Thursday, June 01, 2017

  MFUNGAJI BORA LIGI KUU ATAKA MILIONI 80 AONDOKE JESHINI

  Na Shekha Jamal, DAR ES SALAAM
  MFUNGAJI bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Abdulraman Mussa amesema kwamba yupo tayari kuondoka Ruvu Shooting iwapo itatokea timu ya kumpatia dau la Sh. Milioni 80.
  Abdulrahaman ameonyesha kiwango kizuri na msimu huu wa Ligi Kuu na kuibuka mfungaji bora akiwa amefunga mabao 14 sawa na Saimon Msuva wa Yanga.
  Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa kutakiwa na timu ya Stand United pamoja na Azam FC kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Bara.
  Abdulraman Mussa (katikati) akiwa ameshika tuzo yake ya mfungaji bora wa Ligi Kuu pamoja na viongozi wake wa Ruvu Shooting  

  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo kwa simu kutoka Alexandria, Misri ambako yupo na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa kujiandaa na mchezo wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi la Lesotho Juni 10, mwaka huu, Mussa amesema yupo tayari kuachana na timu yake hiyo akipewa kiasi cha Million 80 ili kuachana na ajira yake ya jeshi.
  Alisema hadi sasa hakuna timu iliyomfuata lakini kwa upande wake hataweza kuacha ajira kwa dau dogo hivyo kama timu itamuhitaji kwa dau hilo.
  "Kwanza watambue ninaajira hivyo kama kuna timu itanipa dau hilo kwangu bila shaka nitavua gwada na kucheza soka katika timu hiyo," alisema Abdulrahaman.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MFUNGAJI BORA LIGI KUU ATAKA MILIONI 80 AONDOKE JESHINI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top