• HABARI MPYA

    Wednesday, June 21, 2017

    ARSENAL YATAKA KUMALIZANA NA AARON RAMSEY MAPEMA

    KLABU ya Arsenal haitaki kurudia makosa na sasa inataka kumsainisha mkataba mpya Aaron Ramsey mapema.
    The Gunners iliruhusu wachezaji wake kadhaa nyota kufikisha miezi 12 ya mwisho kuelekea mwisho wa mikataba yao: Alexis Sanchez, Mesut Ozil, Alex Oxlade-Chamberlain, Kieran Gibbs na Jack Wilshere wakiwa miongoni mwao ambao wanaweza kuondoka bure Emirates msimu ujao.
    Kwa kushindwa kuwabana mapema kwa mikataba wachezaji hao, Arsenal inajiweka kwenye mazingira ya kutumia fedha nyingi msimu ujao kusajili iwapo nyota hao hata baadhi yao tu wataondoka bure. 
    Arsenal inataka kumsainisha mkataba mpya mapema Aaron Ramsey ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2019 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

    Ndani ya Uwanja wa Emirates hatua zimechukuliwa na uteuzi wa Huss Fahmy katika uongozi kutoka timu ya Sky kushughulikia mikataba ni moja ya mikakati ya kuhakikisha hilo halitokei.
    Daniel Levy hajaruhusu wachezaji wake kufika miaka miwili ya mwisho ya mikataba yao kuhakikisha Tottenham haijiweki katika presha, na sasa The Gunners wanafuata utaratibu huo.
    Bin Zubeiry Sports - Online inafahamu Ramsey, ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2019, ni wa kwanza kuombwa asaini mkataba mpya.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Wales kwa sasa analipwa Pauni 100,000 kwa wiki na katika mkataba mpya anatarajiwa kulipwa sawa na Ozil na Sanchez wanaolipwa zaidi klabuni.
    Danny Welbeck, Theo Walcott na Petr Cech mikataba yao pia inamalizika mwaka 2019 na wanaweza kufuatia katika mazungumzo ya mikataba mipya. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YATAKA KUMALIZANA NA AARON RAMSEY MAPEMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top