• HABARI MPYA

    Tuesday, June 20, 2017

    MALIMA 'JEMBE ULAYA' NA WENGINE 73 WAREJESHA FOMU KUWANIA UONGOZI TFF

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WATU 74 akiwemo beki wa zamani wa Yanga, Bakari 'Jembe Ulaya' Malima wamechukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma.
    Hadi zoezi hilo linafungwa leo Juni 20, 2017 saa 10.00 jioni wagombea wote wamerejesha ambako kwenye nafasi ya urais, jumla ya wagombea 10 walijitokeza kuomba nafasi hiyo wakati kwenye makamu rais wamejitokeza sita.
    Wadau 58 wamejitokeza kuwania nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji katika Katika Kanda mbalimbali. Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu kwa mujibu wa Kanuni ya 10, limefanyika kwa siku tano kuanzia Juni 16, 2017 hadi Juni 20, mwaka huu.
    Beki wa zamani wa Yanga, Bakari 'Jembe Ulaya' Malima amerejesha fomu za kuwania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF 

    Siku ya kwanza ilipoanza tu, Jamal Malinzi alikuwa wa kwanza kuchukua fomu na kurejesha huku akifuatiwa na Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Athumani Nyamlani, Fredrick Mwakalebela, John Kijumbe, Shija Richard, Ally Mayay na Emmanuel Kimbe.
    Waliojitokeza kuwania Makamu wa Rais na kurejesha fomu wako Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa.
    Kwa siku tatu, kuanzia kesho, Kamati ya Uchaguzi itaanza mchujo wa awali kwa wote waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali kwa mujibu wa kanuni ya 11.1 ya Uchaguzi wa TFF.

    Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa kufuata Kanda 13 ni kama ifuatavyo:
    Kanda Na. 1 Mikoa ya Kagera na Geita; Salum Chama, Kaliro Samson, Leopold 'Taso' Mukebezi na Abdallah Mussa.
    Kanda Na. 2 Mikoa ya Mara na Mwanza; Vedastus Lufano, Ephraim Majige, Samuel Daniel na Aaron Nyanda.
    Kanda Na. 3 Mikoa ya Shinyanga na Simiyu; Benista Rugora, Mbasha Matutu na Stanslaus Nyongo.
    Kanda Na. 4 Mikoa ya Arusha na Manyara; Omari Walii, Sarah Chao na Peter Temu.
    Kanda Na. 5 Mikoa ya Kigoma na Tabora; John Kadutu, Issa Bukuku, Abubakar Zebo na Francis Michael. Kanda Na. 6 Mikoa ya Katavi na Rukwa; Kenneth Pesambili na Baraka Mazengo.
    Kanda Na. 7 Mikoa ya Mbeya, Songwe na Iringa; Elias Mwanjala, Cyprian Kuyava, Erick Ambakisye na Abousuphyan Silliah.
    Kanda Na. 8 Mikoa ya Njombe na Ruvuma; James Mhagama, Golden Sanga, Vicent Majili na Yono Kevela. Kanda Na. 9 Lindi na Mtwara; Athuman Kambi na Dunstan Mkundi.
    Kanda Na. 10 Mikoa ya Dodoma na Singida; Hussein Mwamba, Mohamed Aden, Mussa Sima, Stewart Masima, Ally Suru na George Benedict.
    Kanda Na. 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro; Charles Mwakambaya, Gabriel Makwawe, Francis Ndulane na Hassan Othman ‘Hassanol’. 
    Kanda ya 12. Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga; Khalid Mohamed, Goodluck Moshi na Thabit Kandoro.
    Kanda Na. 13 Mkoa wa Dar es Salaam; Emmanuel Ashery, Ayoub Nyenzi, Saleh Alawi, Shaffih Dauda, Abdul Sauko, Peter Mhinzi, Ally Kamtande, Said Tully, Mussa Kisoky, Lameck Nyambaya, Ramadhani Nassib, Aziz Khalfan, Jamhuri Kihwelo, Saad Kawemba na Bakari Malima.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALIMA 'JEMBE ULAYA' NA WENGINE 73 WAREJESHA FOMU KUWANIA UONGOZI TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top