• HABARI MPYA

    Friday, June 30, 2017

    KICHUYA AWANIA ‘KIATU CHA DHAHABU’ COSAFA 2017

    Na Mwandishi Wetu, RUSTERNBURG
    WINGA wa Tanzania, Shiza Ramadhani Kichuya anachuana na Mzimbabwe, Ovidy Obvious Karuru kuwania ufungaji bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA), Castle.
    Mchezaji huyo wa Simba SC ya Dar es Salaam, ana mabao mawili hadi sasa sawa na Karuru anayechezea AmaZulu ya Daraja la Kwanza nchini Afrika Kusini.
    Hatua ya makundi ya michuano hiyo inahitimishwa leo kwa mechi za Kundi B, kati ya Msumbiji na Madagascar Uwanja wa Moruleng na Zimbabwe na Shelisheli Uwanja wa Royal Bafokeng, mechi zote zikianza Saa 12:00 jioni.
    Shiza Kichuya wa Tanzania (kushoto) anawania ufungaji bora Kombe la COSAFA Castle
    Tayari Tanzania imefuzu Robo Fainali baada ya kuongoza Kundi A na itamenyana na wenyeji, Afrika Kusini Jumapili Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace kuanzia Saa 12:00 jioni.
    Robo fainali nyingine itazikutanisha Botswana na Zambia Saa 10:00 jioni Royal Bafokeng Sports Palace na Namibia dhidi ya Lesotho Saa 12:00 jioni, wakati mechi nyingine ya Jumapili itakuwa kati ya Swaziland na mshindi wa Kundi B Saa 2:00 usiku Royal Bafokeng pia.
    Kutakuwa na hatua mbili za Nusu Fainali na Fainali, ikizihusisha timu zote, zilishinda zikiendelea COSAFA Castle na zilizofungwa zikihamia kwenye michuano ya Plate kuchuana na hadi bingwa kupatikana.
    Mbali na Kichuya na Ovidy Karuru kuwa na mabao mawili kila mmoja, wengine waliofanikiwa kufunga bao moja kila mmoja hadi sasa ni Blessing Majarira (Zimbabwe), Roddy Melanie (Shelisheli), Ocean Mushure (Zimbabwe), Saimon Msuvu (Tanzania), Mutong (Msumbiji), Augusto Quibeto (Angola), Joseph Perticots (Mauritius), Rinjala Raherinaivo (Madagascar), Ardino Raveloarisona (Madagascar) na Stelio (Msumbiji).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KICHUYA AWANIA ‘KIATU CHA DHAHABU’ COSAFA 2017 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top