• HABARI MPYA

    Sunday, June 25, 2017

    RONALDO AFUNGA, URENO YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MABARA

    Cristiano Ronaldo akishangilia kibabe baada ya kuifungia Ureno bao la kwanza kwa penalti dakika ya 33 katika ushindi wa 4-0 dhidi ya New Zealand baada ya Danilo kuchewa rafu usiku wa Jumamosi Uwanja wa Krestovskyi mjini St Petersburg katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mabara. Mabao mengine ya Ureno yalifungwa na Bernardo Silva dakika ya 37,  Andre Silva dakika ya 80 na Luis Nani dakika ya 90 na ushei. Matokeo hayo yanaifanya Ureno ifikishe pointi saba na kumalizana kileleni sawa na Mexico iliyomaliza na pointi saba pia baada ya kuifunga Urusi 2-1 na zote zinakwenda Nusu Fainali. Wenyeji Urusi wameungana na New Zealand kupanda jukwaani kitazama mechi za kumalizia michuano ya 2017 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO AFUNGA, URENO YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MABARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top