• HABARI MPYA

    Wednesday, June 28, 2017

    MTIBWA SUGAR YAMTEMA BAHANUZI, YASAJILI WAWILI WAPYA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WAFALME wa zamani wa soka ya Tanzania, Mtibwa Sugar wamesajili wachezaji wapya wawili chipukizi, ambao ni beki wa kati, Hussein Iddi na mshambuliaji Salum Ramadhani huku ikiwaruhusu kuondoka wachezaji saba waliomaliza mikataba akiwemo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Said Bahanuzi.
    Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba Hussein Idd ametokea JKT Oljoro ya Arusha na Salum Ramadhani anayefahamika kwa jina la utani, Chuji ametokea Polisi Morogoro.
    Bayser, amesema kwamba wachezaji hao wamesaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja na ni matumaini ya Mtibwa Sugar watang’ara Manungu.
    Said Bahanuzi ameruhusiwa kuondoka Mtibwa Sugar baada kumaliza mkataba wake 
    Pamoja na hayo, Bayser amesema kwamba wanatarajia benchi la Ufundi chini ya Kocha Mkuu Zubeiry Katwila kupandisha baadhi ya wachezaji kutoka katika timu ya vijana ya Mtibwa Sugar.
    “Uongozi wa Mtibwa Sugar unaendelea kufanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi, hivyo basi usajili bado unaendelea na nyota wengine wanatarajiwa kuingia makubaliano na Mtibwa Sugar wakati wowote kuanzia sasa,”amesema.
    Wachezaji wapya waliosajiliwa Mtibwa Sugar, Salum Ramadhani 'Chuji' (kushoto) na Hussein Iddi (kulia)

    Aidha, Bayser amesema kwamba Mtibwa Sugar imeachana na Jaffary Salum Kibaya, Said Mkopi, Maulid Gole ‘Adebayor’, Said Bahanuzi, Vincent Barnabas, Ally Lundenga na Ally Shomary ambao wamemaliza mikataba yao.
    Mtibwa inasifika mno kwa kuibua wachezaji chipukizi kutoka timu mbalimbali ndogo na wengine kupandisha kutoka kikosi chake cha vijana ambao baadaye hugeuka lulu na kugombewa na timu kubwa, hususan Simba na Yanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAMTEMA BAHANUZI, YASAJILI WAWILI WAPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top