• HABARI MPYA

    Thursday, June 15, 2017

    MAN UNITED YASAJILI BEKI MREFU FUTI SITA KUTOKA BENFICA

    Manchester United imekamilisha usajili wa beki wa Benfica, Victor Lindelof PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


    WASIFU WA LINDELOF 

    Kuzaliwa: Julai 17, 1994 mjini Vasteras, Sweden (Miaka 22)
    Urefu: Futi 6 inchi 2
    Nafasi: Beki wa kati/ Beki wa kulia
    REKODI YA KLABU 
    2010-2012: Vasteras mechi 41, mabao 0
    2012-2016: Benfica B mechi 96, mabao 4
    2013-2017: Benfica mechi 73, mabao 2
    2017-: Manchester United 
    Rekodi ya timu ya taifa
    2016-: Sweden mechi 12, bao 1
    TIMU ya Manchester United imekamilisha usajili wa beki Victor Lindelof mwenye urefu wa futi sita kutoka Benfica ya Ureno baada ya kufuzu vipimo vya afya.
    Lindelof, ambaye ameigharimu United Pauni Milioni 30.7, aliwasili viwanja vya mazoezi vya klabu, Carrington Jumatanop asubuhi.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa akisakwa na kocha wa United, Jose Mourinho kwa muda mrefu.
    Mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden ameelezea furaha yake kutua Old Trafford.
    Inafahamika pia Benfica inaweza kupata Pauni Milioni 8.8 zaidi.
    Katika mahojiano na tovuti rasmi ya klabu, amesema: "Nina furaha kujiunga na Manchester United. Nimefurahia wakati wangu nikiwa Benfica na nimejifunza mengi huko. Lakini naangalia mbele namna ya kucheza Ligi Kuu nikiwa Old Trafford na Jose Mourinho,"amesema. 
    Mchezaji anatarajiwa kuanza kujumuika kucheza na wachezaji wenzake wapy katika ziara ya Marekani kujiandaa na msimu na Mourinho anaamini Lindelof ataongeza tija katika katika safu yake ya ulinzi hususan baada ya timu kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED YASAJILI BEKI MREFU FUTI SITA KUTOKA BENFICA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top