• HABARI MPYA

    Sunday, February 22, 2026

    AZAM FC ‘YAICHIMBIA KABURI’ KMC, YAICHAPA 2-0 MWENGE


    TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa KMC Complex, Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
    Mabao yote ya Azam FC leo yamefungwa na winga Idii Suleiman Ali – maarufu tu kama Iddi Nado dakika ya 55 na 65 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 19 katika mchezo wa tisa na kupanda kwa nafasi moja hadi ya nane.
    Hali inazidi kuwa mbaya kwa KMC baada ya mchezo wa 12 wa msimu leo – nyingine nne ikishinda mbili na kutoa sare mbili hivyo kuendelea kushika mkia katika Ligi Kuu inayoshirikisha timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.  

    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC ‘YAICHIMBIA KABURI’ KMC, YAICHAPA 2-0 MWENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top