• HABARI MPYA

  Thursday, June 15, 2017

  MAYWEATHER ATHIBITISHA KUZIPIGA NA MCGREGOR AGOSTI 6

  HATIMAYE bondia Floyd Mayweather ametaja tarahe ya kurejea ulingoni kuzipiga na mbabe wa UFC, Conor McGregor.
  Wapiganaji hao wawili watakutana ulingoni Agosti 6, mwaka huu mjini Las Vegas, Marekani katika pambano la utajiri mkubwa.
  Na hilo linatarajiwa kuwa pambano kubwa zaidi katika historia ya michezo ya mapigano tangu Mayweather achapane na Manny Pacquiao.

  Floyd Mayweather amethibitisha atapigana na Conor McGregor Agosti 26 mjini Las Vegas, Marekani PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Hiyo itakuwa mechi ya kwanza ya ngumi za kawaida kwa mbabe wa Ireland kama ilivyo kwa Mayweather kupigana na mtu wa mchezo tofauti kwwa mara ya kwanza siku hiyo.
  Tume ya Michezo ya Nevada imemuhakikishia 'Bwana Fedha' kwamba hawatapewa kikwazo chochote kufanya pambano hilo.
  Mayweather anatarajiwa kupata si chini ya dola za Kimarekani Milioni 100, pamoja na mauzo ya juu Showtime, TV kubwa ya kulipia Marekani, wakati McGregor anaweza kupata dola Milioni 80 ingawa sehemu ya fedha hizo atatakiwa kulipa UFC, chama cha mchezo wa sanaa za mapigano mchanganyiko.
  Rais wa UFC, Dana White ameiambia ESPN: "Tumekuwa kwenye majadiliano kwa muda na kusema kweli majadiliano yamekwenda kiulaini. Tumefanikisha jambo,".
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYWEATHER ATHIBITISHA KUZIPIGA NA MCGREGOR AGOSTI 6 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top