• HABARI MPYA

  Thursday, June 15, 2017

  KAGERA SUGAR YASAJILI SITA WAPYA, NYOSSO NDANI

  Na Shekha Jamal, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Kagera Sugar ya Bukoba imesajili wachezaji sita wapya, akiwemo beki wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba, Juma Said Nyosso (pichani kushoto).
  Nyosso anasajiliwa Kagera Sugar baada ya kumaliza adhabu yake ya kufungiwa miaka miwili kufuatia kumtomasa makalio mshambuliaji John Raphael Bocco akiwa Azam FC kabla ya kuhamia Simba wiki hii. 
  Mbali na Nyosso ambaye alifungiwa akiwa anachezea Mbeya City mwaka juzi, Kagera Sugar pia imemsajili kipa Hussein Kipao kutoka JKT Ruvu iliyoshuka Daraja kutoka Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita.  
  Japhary Kibaya ametua Kagera Sugar ya Bukoba kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro

  Wengine ni beki Japhary Kibaya kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, viungo Peter Samson Mwalyanzi, Ludovic Venance na mshambuliaji Omary Daga maarufu ‘Dagashenko’ wote kutoka Africa Lyon iliyoshuka Daraja pia.
  Tayari Kagera Sugar imempoteza mshambuliaji wake tegemeo, Mbaraka Yussuf Abeid aliyesaini Azam FC wiki iliyopita, huku pia kiungo Babu Ally Seif akiripotiwa kuwa mbioni kujiunga na Yanga. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YASAJILI SITA WAPYA, NYOSSO NDANI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top