• HABARI MPYA

  Saturday, April 08, 2017

  SAMATTA ACHEZA MECHI YA 50 GENK YASHINDA 1-0

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku huu amecheza mechi yake 50 KRC Genk ikishinda 1-0 ugenini dhidi ya KSV Roeselare katika mchezo wa kuwania kucheza michuano ya Europa League msimu ujao Uwanja wa Schiervelde mjini Roeselare, Ubelgiji.  
  Bao pekee la Genk limefungwa na mshambuliaji kutoka Hispania, Jose Naranjo dakika ya 84, dakika tatu tu baada ya kuingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya Mbelgiji, Leandro Trossard. 
  Baada ya kufunga mabao sita katika mechi tano zilizopita za Genk, leo Nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta aliwekewa ulinzi mkali na mabeki wa KSV Roeselare. 
  Leo Samatta amecheza mechi ya 50 tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana akitokea TP Mazembe ya DRC, akiwa amefunga jumla ya mabao 18.
  Kati ya mechi hizo 50, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 32 msimu huu na kati ya hiyo, ni michezo 31 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 20 msimu huu.
  Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita msimu huu na katika mabao hayo 18, 12 amefunga msimu huu na sita msimu uliopita.
  Kikosi cha KSV Roeselare kilikuwa: Biebauw, Schmisser, Seoudi/Van Acker dk82, Lecomte, Kehli, Godwin/Cornet dk74, Damman, Zolotic, Grisez, Lepicier na Van Eenoo/Ibou dk78.
  KRC Genk: Ryan, Uronen, Colley, Brabec, Castagne, Berge, Malinovskyi/Heynendk45, Pozuelo, Trossard/Naranjo dk80, Boetius/Buffalo dk63 na Samatta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA ACHEZA MECHI YA 50 GENK YASHINDA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top