• HABARI MPYA

    Wednesday, April 26, 2017

    MAMELODI, MAZEMBE ZAPANGWA ‘MAKUNDI YA KIFO’ AFRIKA

    MABINGWA watetezi, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini wamepangwa Kundi C katika Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Esperance ya Tunisia, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Saint-George ya Ethiopia.
    Katika droo iliyopangwa leo mjini Cairo, Misri yalipo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), mabingwa mara nyingi zaidi wa Kombe hilo, Al Ahly ya Misri waliotwaa taji hilo mara nane katika miaka ya 1982, 1987, 2001, 2005, 2006, 2008, 2012 na 2013 wameangukia Kundi D.
    Vigogo hao wa Misri wamepangwa pamoja na mabingwa wa mwaka 1992, Wydad Athletic Club ya Morocco, Coton Sport ya Cameroon na Zanaco ya Zambia.
    Zamalek ya Misri wanaofuatia Ahly kutwaa marab nyingi taji hilo, wakiwa wamebeba mara tano sawa na TP Mazembe ya DRC, wamepangwa Kundi B pamoja na USM Alger ya Algeria, Ahli Tripoli ya Libya na Caps United ya Zimbabwe.
    Kundi A lina timu za Etoile du Sahel ya Tunisia mabingwa wa mwaka 2007, vigogo wa Sudan, El Hilal na El Merreikh na mabingwa wa Msumbiji, Ferroviario Beira.
    Katika Kombe la Shirikisho, KCCA ya Uganda imepangwa Kundi A pamoja na FUS Rabat ya Morocco, Club Africain ya Tunisia na Rivers United ya Nigeria.
    Mabingwa watetezi TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamepangwa Kundi D pamoja na Supersport United na Afrika Kusini na Horoya AC ya Guinea na CF Mounana ya Gabon.
    CS Sfaxien imepangwa Kundi B pamoja na Platinum Stars, MC Alger na Mbabanwe Swallows wakati Zesco United ya Zambia imepangwa Kundi C pamoja na Recreativo do Libolo ya Angola, Al Hilal Elobeid ya Sudan na Smouha ya Misri.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAMELODI, MAZEMBE ZAPANGWA ‘MAKUNDI YA KIFO’ AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top