• HABARI MPYA

  Thursday, September 01, 2016

  HUMUD APATA TIMU AFRIKA KUSINI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa zamani wa Simba SC na Azam FC, Abdulhalim Humud ‘Gaucho’ amejiunga na klabu ya Real Kings FC ya Ligi Daraja la Kwanza Afrika Kusini.
  Humud ambaye msimu uliopita alichezea Coastal Union ya Tanga iliyoshuka daraja kutoka Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na timu ya Durban, Kwazulu-Natal.
  Real Kings walipanda Ligi Daraja la Kwanza mwaka huu na wakafanikiwa kufika fainali ya ligi ya ABC Motsepe League.
  Wakala aliyefanikisha Humud kusaini Real Kings, amesema leo kwa simu kutoka Durban kwamba ana matumaini mchezaji huyo atafanya vizuri Afrika Kusini.
  Abdulhalim Humud (kushoto) akipambana na kiungo wa Yanga, Deus Kaseke msimu uliopita

  “Namjua vizuri Humud, kuna wakati alikuja Jomo Cosmos hapa kucheza. Ni mchezaji mzuri na nina matumaini atafanya vizuri tena hapa,”alisema Mathaba.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HUMUD APATA TIMU AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top