• HABARI MPYA

    Thursday, September 01, 2016

    FIFA SASA YALETA GPX KATIKA MFUMO WA USAJILI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA), limesambaza waraka mpya kwa wanachama wake, likiwamo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ukisema mameneja wote wa usajili wa wachezaji kwa mfumo wa Mtandao (TMS-Transfer Matching System Managers) hawana budi kujiunga na mawasiliano mapya ili kupata taarifa mbalimbali za usajili na uhamisho wa wachezaji.
    FIFA limeleta mfumo huo unaoitwa GPX yaani Global Players Exchange ambao malengo yake ni kurahisisha kufanya usajili kwa mchezaji mmoja kwenda timu nyingine, lakini kabla ya kufanya hivyo utasaidia kupata taarifa kamili za mchezaji huyo na shabaha kuu ni kurahisisha mawasiliano ya TMS Managers nchi nzima, klabu na mashirikisho mbalimbali duniani.

    Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akiwa na Rais wa FIFA, Gianni Infantino 

    GPX ni kama mtandao wa kijamii unaoweza kulinganishwa na ‘WhatsApp’ unaofanya kuwa na mawasiliano ya karibu na FIFA imeagiza kuwa ni lazima mameneja wa TMS wa kila klabu na mashirikisho ya ya mpira wa miguu kujiunga na mtandao huo ambao si tu kwamba utafanya kazi katika nchi husika, bali pia unaunganisha ulimwengu wote.
    Kwa mameneja wa usajili wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (SFDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) watakaokuwa tayari basi hawana budi kuwasiliana na Meneja Usajili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kupata maelezo ya kina ya namna ya kujiunga na mtandao wa GPX.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FIFA SASA YALETA GPX KATIKA MFUMO WA USAJILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top