• HABARI MPYA

  Tuesday, August 02, 2016

  KWIZERA ASAINI MKATABA MPYA RAYON

  KIUNGO wa kimataifa wa Burundi, Pierre Kwizera amesaini Mkataba mpya wa miaka miwili na Rayon Sport baada ya mwishoni mwa wiki kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa msimu wa 2015/16 wa Ligi Kuu ya Azam Rwanda. 
  Katika sherehe zilizofanyika mjini kigali, Ijumaa ya Julai 29, mabingwa wa Ligi Kuu ya Rwanda msimu wa 2015/16, APR pia walikabidhiwa zawadi zao.
  Kiungo mshambuliaji wa Rayon Sport, Kwizera alifanikiwa kushinda tuzo hiyo akiwaangusha wachezaji mwenzake Savio Dominique Nshuti na Muhadjir Hakizimana aliyehamia APR kutoka Mukura Victory Sports.
  “Nawashukuru wachezaji wenzangu na kocha (Djuma Masudi). Tunatakiwa kujituma zaidi kwa ajili ya msimu ujao. Tulijitahidi kushindania taji na tutaendeleza nguvu hiyo msimu ujao,” alisema Kwizera.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aliyejiunga na The Blues Januari 2015 kutoka Simba ya Tanzania amefunga mabao saba msimu uliopita na alikuwa tegemeo la Rayon katika safu ya kiungo, akiiwezesha kushika nafasi ya pili kwenye Ligi na kutwaa Kombe Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA), maarufu kama Peace Cup.
  Kwizera akasaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kufanya kazi na Rayon. “Nina furaha na nitaelekeza fikra zangu mbele katika kushinda zaidi. Nitaendelea kujituma kwa timu yangu na kufunga mabao zaidi kqwa ushirikiano na wachezaji wenzangu,” alisema.
  Rayon ilitawala usiku wa tuzo za ligi ikiwemo kocha wake, Djuma Masudi kushinda tuzo ya Kocha Bora wa Msimu, akiwabwaga Mtunisia wa APR, Nizar Khanfir na Innocent Seninga wa  Etincelles FC.
  mshambuliaji Savio alishinda tuzo ya Mchezaji Bora Anayechipukia, wakati Eric ‘Bakame’ Ndayishimiye ameshinda tuzo ya Kipa Bora.

  Kwizera katikati akipokea tuzo yake mwishoni mwa wiki mjini Kigali

  WASHINDI WA TUZO:
  Mchezaji Bora: Pierrot Kwizera (Rayon Sport)
  Mfungaji Bora: Hakizimana Muhadjiri (Mukura VS) na Danny Usengimana (Police FC) kila mmoja mabao 16
  Mchezaji Bora Chipukizi: Savio Dominique Nshuti (Rayon Sports)
  Kipa Bora: Eric Ndayishimiye (Rayon Sport)
  Kocha Bora: Eric Nshimiyimana (AS Kigali)
  Kocha Bora mpya: Djuma Masudi (Rayon Sport)
  Refa Bora: Louis Hakizimana
  Mshika Kibendera Bora: Zephanie Niyonkuru

  Eric Ndayishimiye amekuwa kipa bora wa Ligi Kuu ya Rwanda 

  Kikosi cha Bora;
  Kipa: Eric Ndayishimiye (Rayon Sport)
  Mabeki: Fitina Ombolenga (SC Kiyovu), Emmanuel Imanishimwe (Rayon Sport), Fiston Munezero (Rayon Sport) and Abdul Rwatubyaye (APR)
  Viungo:  Pierrot Kwizera (Rayon Sport), Ally Niyonzima (Mukura VS), Muhadjiri Hakizimana (Mukura VS), Savio Dominique Nshuti (Rayon Sport) and Iranzi Jean Claude (APR FC)
  Mshambuliaji: Ismailia Diarra (Rayon Sport)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KWIZERA ASAINI MKATABA MPYA RAYON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top