• HABARI MPYA

  Thursday, August 04, 2016

  KILA LA HERI MBWANA SAMATTA EUROPA LEAGUE LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta leo atakuwa anawania tiketi ya kwenda hatua ya makundi ya Europa League wakati timu yake, KRC Genk itakapomenyana na wenyeji Cork City FC katika mchezo wa marudiano Raundi ya Tatu ya mchujo.
  Genk inahitaji kulazimisha sare kesho Uwanja wa Turner's Cross, mjini Cork, Ireland baada ya awali kushinda 1-0 Alhamisi iliyopita nyumbani.
  Na pamoja na ugumu uliopo mbele yao, Samatta alisema; “Lakini tutapambana, maana yake kwenye mchezo wa marudiano tunatakiwa kwenda kutafuta mabao na kujilinda, tutajitahidi,”.
  Mbwana Samatta (katikati) akifurahia na wenzake baada ya kufunga mechi iliyopita

  Katikati ya Julai Samatta aliiongoza timu yake, Genk kuitoa Buducnost ya Montenegro kwa penalti 4-2, baada ya sare ya jumla ya 2-2, kilatimu ikishinda 2-0 nyumbani kwake, anatarajiwa kuanza kesho
  Timu hizo zilifikia kwenye matuta baada ya sare ya jumla ya 2-2, Genk ikianza kushinda 2-0, mabao ya Neeskens Kebano kwa penalti dakika ya 16 na Samatta dakika ya 79 Alhamisi wiki iliyopita kabla ya Buducnost kulipa kisasi kwa ushindi wa 2-0, mabao ya Radomir Dalovic dakika ya kwanza na Milos Raickovic dakika ya 39.
  Katika mikwaju ya penalti, waliofunga upande wa Genk ni Thomas Buffel, Bryan Heynen, Samatta na Dries Wouters ya mwisho, wakati za Buducnost zilifungwa na Risto Radunovic na Radomir Dalovic, huku Momcilo Raspopovic na Luka Mirkovic wakikosa.
  Ikumbukwe timu zitakazoshinda zitakwenda hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi, ambako vigogo kama Manchester United ya England wataanzia huko.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KILA LA HERI MBWANA SAMATTA EUROPA LEAGUE LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top