• HABARI MPYA

  Wednesday, May 04, 2016

  TFF YAAFIKI UCHAGUZI YANGA KUSOGEZWA MBELE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetangaza Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Yanga kuwa utafanyika Juni 25, 2016 badala ya Juni 5, 2016.
  Kamati ya Uchaguzi ya TFF imelazimika kufanya hivyo kwa kuzingatia ushiriki wa Yanga ambayo inashiriki michuano ya kimataifa.
  Sekretarieti ya Yanga ambayo ingefanya kazi kwa pamoja na Kamati ya Uchaguzi kwa kushirikiana na TFF kwa sasa inashughulikia pia kuiandaa timu kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

  Yanga inatarajiwa kucheza na Esperanca ya Angola katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Mei 7, mwaka huu kabla ya kurudiana kati ya Mei 17 na 18, mwaka huu huko Angola.
  Kwa mujibu wa ratiba mpya, fomu za kuwania uongozi wa Yanga zitaanza kuchukuliwa Mei 25, 2016 na kwamba uchaguzi huo utafanyika ndani ya muda ambao Serikali kwa kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) iliagiza uchaguzi kufanyika kabla ya Juni 26, 2016 hivyo uchaguzi utafanyika ndani ya wakati.
  Katiba itakayotumika ni ya mwaka 2010 na kwamba Wanachama wa Yanga watatumia kadi za kawaida za uanachama na si za benki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAAFIKI UCHAGUZI YANGA KUSOGEZWA MBELE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top